• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu waziri mkuu wa China akutana na mkuu wa Benki Kuu ya Dunia

    (GMT+08:00) 2018-11-03 17:17:48

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He amekutana na mkuu wa Benki Kuu ya Dunia Bw. Kim Yong aliyekuja China.

    Bw. Liu amesema mwaka huu ukiwa ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango , maonesho ya kwanza ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China yatakayofanyika mjini Shanghai ni tangazo na utekelezaji wa sera kubwa ya kufungua soko, na China ina nia ya kuimarisha ushirikiano wa wenzi wa maendeleo na Benki Kuu ya Dunia, kuendelea kuboresha usimamizi wa uchumi wa kimataifa na kuhimiza kwa pamoja utandawazi wa uchumi na maendeleo endelevu.

    Kwa upande wake Bw. Kim Yong amesema kuwa Benki Kuu ya Dunia imepongeza mafanikio makubwa ya China katika sekta ya mageuzi na ufunguaji mlango na maendeleo ya kupunguza umaskini. Aidha imeishukuru China kwa kutoa mchango kwa Benki Kuu ya Dunia, na ina nia ya kuendelea kuimarisha ushirikiano husika wa pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako