• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping akutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini Shanghai

    (GMT+08:00) 2018-11-04 19:50:32

    Rais Xi Jinping wa China leo huko Shanghai amekutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

    Rais Xi amemkaribisha rais Kenyatta kwenye Maonesho ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China, amesema China inapenda kuisaidia Kenya kuongeza uwezo wa ushindani wa bidhaa zake, na kupanua uagizaji wa bidhaa kutoka Kenya.

    Rais Kenyatta amesema anatarajia kuimarishwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Kenya na China kupitia maonesho hayo. Amesema Kenya inapenda kuimarisha ushirikiano na China kwenye uchumi na biashara, kilimo na ujenzi wa miundo mbinu, na kuweka mazingira mazuri kwa kampuni za China kuwekeza nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako