• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China na mkewe Peng Liyuan wakaribisha wageni kwenye maonyesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje CIIE

    (GMT+08:00) 2018-11-05 07:34:24

    Rais Xi Jinping wa China na mkewe Bibi Peng Liyuan jana usuku walifanya hafla ya kuwakaribisha wageni wa heshima wanaohudhuria maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje (CIIE) mjini Shanghai, China. Rais Xi alitoa hotuba ya kuwakaribisha viongozi na wageni kutoka nchi mbalimbali, akisema,

    "Maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje ni maonyesho ya China, hasa kwa nchi zote duniani, na si maonyesho ya kawaida, ni uamuzi muhimu wa China katika kuhimiza sera ya ufunguaji mlango kwa kiwango cha juu, pia ni hatua muhimu ya China katika kufungua soko lake kwa hiari kwa nchi zote duniani."

    Rais Xi amesema wageni wa nchi mbalimbali watafanya mawasiliano juu ya masuala makuu ya mambo ya uchumi na biashara ya dunia, na utaratibu wa usimamizi wa uchumi wa dunia.

    "Maonyesho haya yatakayotuletea matarajio mengi, yatawanufaisha wananchi wa nchi mbalimbali. Naamini kuwa chini ya uungaji mkono na jitihada za pande zote, maonyesho hayo yatakuwa maonyesho ya kimataifa yenye kiwango cha juu, pia yatatoa mchango mkubwa katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na biashara ya kimataifa, kuhimiza pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', kuhimiza kujenga jukwaa jipya kwa mafungamano ya kiuchumi, kuzidi kuwanufaisha wananchi wa dunia, na kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja."

    Wakati huo huo, rais Xi amekutana na rais Kenyatta wa Kenya, na kufikia makubaliano naye kwenye kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi mbili. Rais Xi amesema China na Kenya zinapaswa kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote upate maendeleo kwa kutumia fursa ya matokeo ya mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC na ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    "Kuja kwako kumeonyesha uungaji mkono wako kwa maonyesho haya, pia kumeonyesha unatilia maanani uhusiano kati ya nchi zetu mbili. Nakupongeza sana. Natumai Kenya itatumia vizuri fursa hii na kuonyesha bidhaa za kienyeji zenye sifa na ubora, na kupanua ushirikiano wa kibiashara kati ya pande zote mbili."

    Rais Kenyatta amesema Kenya inapongeza hatua kubwa inayochukuliwa na China ya kufungua kwa hiari masoko yake, na kuipa kipaumbele Afrika katika mchakato huo. Amesema Kenya inapenda kushirikiana na China kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya Afrika na China, kulinda ushirikiano wa pande nyingi na mfumo wa biashara huria na kuchangia ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Anasema,

    "Tunatarajia kushiriki kwenye maonyesho haya ya kusisimua, na pia tunapenda kutumia fursa hii kuzidisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Kenya na China. Nakubaliana na rais Xi kuhusu mtazamo wake kuwa maendeleo ni msingi wa kutatua matatizo yote, napongeza pendekezo la ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kutilia maanani makubaliano ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kwani hatua hizo zitatoa mchango muhimu katika kuhimiza amani na maendeleo ya pamoja ya dunia."

    Wafanyabiashara kutoka Kenya wamewasili mjini Shanghai kwa ajili ya maonesho hayo yanayoanza leo. Maonesho haya ya siku tano yanatoa fursa kwa wafanyabiashara kukutana na wateja na pia kutafuta wateja nchini China. Awali mwandishi wetu wa Nairobi Ronald Mutie aliongea na baadhi ya wakenya wanaoshiriki maonesho hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako