• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi Kuu Tanzania Bara: Mzunguko wa 10 umeanza kutoa mwelekeo wa ligi

    (GMT+08:00) 2018-11-05 09:00:22
    Wakati wadau wa soka Tanzania bara wakiendelea kujadili matokeo ya michezo iliyopigwa wikiendi kwenye viwanja tofauti, Yanga ya Dar es salaam imevutwa shati na Ndanda FC kwa kulazimishwa sare ya 1-1 katika mchezo uliochezwa jana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Muda nao unaonekana siyo rafiki tena kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa 2018/19 umefikia katikati, ambapo timu nyingi zina wastani wa michezo zaidi ya 10 sawa a nusu ya michezo yote inayotakiwa kuchezwa na kila timu kabla ya kufikia tamati ya mzuguko wa kwanza.

    Kwa mantiki hiyo, muda si mrefu kuanzia sasa ligi hiyo itasmama kwa muda kutoa nafasi kwa wachezaji kupumzika na kuruhusu zoezi la usajili wa dirisha dogo kwa kila timu itakayohitaji kufanya hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako