• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sakata la Bolt na Klabu ya Central Coast Marines: Bolt asepa

    (GMT+08:00) 2018-11-05 09:01:13
    Ndoa ya muda kati ya nyota Usain Bolt na klabu ya Central Coast Mariners kutoka Australia imevunjika mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kambi ya mfalme huyo wa mbio fupi kushikilia kwamba anastahili kupewa donge nono.

    Wakala wa Usain Bolt, Ricky Simms alitaka mteja wake apewe mkataba wa Shilingi milioni 213.3, lakini ripoti zinasema klabu hiyo kutoka Ligi Kuu ilikuwa tayari kumpa asilimia tano pekee yaani shilingi milioni 10.6 kwa sababu haikuridhishwa sana na kipaji chake.

    Mwanariadha huyu wa rekodi ya mbio za dunia ya amekuwa akifanyiwa majaribio na klabu hiyo tangu awasili mwezi Agosti. Alitumai kutimiza ndoto yake ya utotoni ya kuwa mwanakabumbu bora. Ziara hiyo ya Bolt, 32, ilipata umaarufu kote duniani. Iliongezeka hata zaidi pale alipofuma wavuni mabao mawili katika mechi ya Mariners ya kujiandaa kwa msimu mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako