• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Riadha: New York Marathon- Keitany ang'ara, Simbu na Kamworor hawajafua dafu

  (GMT+08:00) 2018-11-05 10:10:40

  Bingwa mara nne wa mbio za New York, Mary Keitany amethibitisha kuwa yeye ni malkia wa mbio hizo baada ya kumuongoza mkenya mwenzake Vivian Cheruiyot kushinda Makala ya 48 ya mbio hizo.

  Keitany ametumia muda wa saa 2:22:48 huku akiandika muda bora katika historia ya mashindano hayo, nafasi ya pili imechukuliwa na Vivian nay a tatu imeenda kwa mmarekani Shalane Flanagan.

  Katika hali isiyotarajiwa na wengi, bingwa mtetezi toka Kenya Geoffrey Kamworor amejikuta ameshindwa kutamba mbele ya Waethiopia Lelisa Desisa na Tola Shura. Pia mwanariadha wa Tanzania Alphonce Simbu nae hakufua dafu kwenye mbio hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako