• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga mkataba wa makombora ya masafa ya kati kuwa na pande nyingi

    (GMT+08:00) 2018-11-05 17:26:42

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bi. Hua Chunying leo hapa Beijing amesema, mkataba wa makombora ya masafa ya kati ulifikiwa kati ya Russia na Marekani, na China inakataa Marekani kujiondoa kwenye mkataba huo na inapinga mkataba huo kuhusika na pande nyingi.

    Bi. Hua Chunying amesema, mkataba huo unatoa mchango muhimu katika kuboresha ushirikiano wa kimataifa, kuhimiza mchakato wa kupunguza silaha za nyuklia, na pia unalinda uwiano na utulivu wa mkakati wa dunia.

    Bi. Hua amesisitiza kwamba China inafuata sera ya kujilinda na kuchukua mtazamo wa kujizuia katika kuendeleza nguvu za kijeshi, na haina nia ya kutishia nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako