Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella,kwa Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ,alipotembelea eneo la ujenzi na kuweka saini ya uzinduzi wa ujenzi huo wa viwanda 11.
Alisema kati ya viwanda hivyo 11 kipo kiwanda kikubwa cha kutengeneza saruji ambacho kitakuwa cha kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki na kuzalisha tani milioni saba kwa mwaka na ajira takriban 5,000.
Shigella alisema wawekezaji hao kutoka China wamechagua kuwekeza viwanda hivyo katika kijiji cha Mtimbwani kwa kuwa kuna mazingira mazuri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |