• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mamlaka ya Mapato Kenya yatoa notisi kwa  wasiolipa kodi

  (GMT+08:00) 2018-11-05 19:39:50
  Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA) imetoa notisi kwa maelfu ya watu ambao hawajalipa kodi,ikiwataka kulipa ndani ya wiki mbili au kukabiliwa na faini kubwa na riba katika pesa wanazodaiwa.

  Katika notisi ambayo KRA ilitumia walipa ushuru wiki mbili zilizopita,ilitoa onyoa kwa waliokwepa kulipa ushuru kufanya hivyo kabla ya makataa ya tarehe 9 Novemba au kuchukuliwa hatua zaidi.

  Licha ya notisi hizo kutolewa,walipa ushuru wengine wamelalama wakisema kuwa wametumiwa notisi hizo kimakosa kwani wao wameshalipa ushuru na hawana deni lolote na Mamlaka ya Mapato.

  Hata hivyo KRA imesema notisi hizo ni za mfumo wa kielektroniki kwa muda ambao walipa kodi walikosa kulipa kwa wakati uliowekwa kisheria.

  KRA hivi karibuni ilianzisha mfumo mpya ambao unawatambua walipa kodi,madeni,faini na riba,ambapo baadae maafisa wanapewa majukumu ya kufuatilia na kuhakikisha madeni yanalipwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako