• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • BENKI YA CRDB YAWADHAMINI WANAWAKE WAJASIRIAMALI

  (GMT+08:00) 2018-11-05 19:40:18
  Benki ya CRDB iliwadhamini wanawake zaidi ya 58 waliopo katika kikundi cha Jukwaa la Uwezeshaji kwa jina 'Wanawake Mkoa wa Pwani', ili waweze kushiriki maonyesho ya bidhaa za viwandani yaliyofanyika hivi majuzi katika Viwanja vya Sabasaba, vilivyoko Kibaha, Mkoa wa Pwani.

  Haya yalithibitishwa na Meneja wa CRDB tawi la Kibaha, Rosemary Nchimbi, alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali, wakiwamo Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, Waziri wa Nishati. Dk. Medard Kalemani na wananchi mbalimbali waliokuwa wametembelea maonyesho hayo.

  Nchimbi, alisema kuwa, CRDB iliamua kuwadhamini wajasiriamali hao ili waweze kupata fursa ya kushiriki maonyesho hayo na kutangaza bidhaa zinazotengenezwa kupitia vikundi vyao.

  Pamoja na hayo, Nchimbi aliwataka wajasiriamali ambao wapo nje ya vikundi, kuhakikisha wanajiunga kwa haraka kwenye vikundi ili waweze kufaidika na fursa za mikopo na pamoja na udhamini mwingine unaotolewa na CRDB.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako