• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari na wataalamu wa sekta ya kiuchumi washiriki kwenye maonyesho ya CIIE

    (GMT+08:00) 2018-11-06 09:17:10

    Kongamano la kimataifa la Hongqiao la vyombo vya habari na majopo ya washauri bingwa kwenye sekta ya kiuchumi limefanyika jana mjini Shanghai, China.

    Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya "ujenzi na uenezi wa mwundo wa uchumi wa dunia inayofungua mlango" ni sehemu ya Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje (CIIE), ambalo limewavutia wakurugenzi wa vyombo vya habari na wataalamu wa sekta ya kiuchumi kutoka nchi 79, ambao wanajadili wajibu wa vyombo vya habari na jopo la washauri bingwa, katika hali ya mafungamano ya kiuchumi.

    Washiriki wa kongamona hilo wanaona hotuba iliyotolewa na rais Xi Jinping kuhusu kujenga uchumi wa dunia inayofungua mlango yenye uvumbuzi na ushirikishi, na hatua mpya ya China ya kupanua kufungua mlango imeonyesha dhamira imara ya China katika kuchangia fursa na nchi nyingine. Wamesema vyombo vya habari na majopo ya washauri bingwa kutoka nchi mbalimbali, wanapaswa kubeba wajibu wao kwenye mchakato wa kujenga uchumi wa dunia inayofungua mlango.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako