• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi apongeza maonyesho ya anga ya China

    (GMT+08:00) 2018-11-06 16:06:20

    Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi katika Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya China kuhusu Safari za Anga (Airshow China), ambayo yameanza leo katika mji wa bandari wa Zhuhai, mkoa wa Guangdong, kaskazini mwa China.

    Katika barua hiyo iliyosomwa na mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Li Xi, rais Xi amesema China ina nia ya kuendeleza teknolojia ya safari za anga na anga ya juu kwa kushirikiana na nchi nyingine.

    Rais Xi pia amesema maonyesho hayo yatachochea maendeleo ya teknolojia ya safari za anga na anga ya juu duniani, kuboresha kwa kina mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa, na kuwawezesha watu wote duniani kunufaika na maendeleo ya sekta hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako