• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya Benki ya Dunia yaonesha mazingira ya biashara ya China yameboreshwa kwa udhahiri

    (GMT+08:00) 2018-11-06 16:55:25

    Ripoti kuhusu mazingira ya biashara ya mwaka 2019 ambayo ilitolewa hivi karibuni na Benki ya Dunia imeonesha kuwa, nafasi ya China imepanda kutoka ya 78 hadi 46 duniani, ambayo imeyazidi kwa kiasi kikubwa makundi 32 ya uchumi, na kuwa kundi la uchumi linalopata ongezeko la uchumi kwa kasi zaidi ndani ya mwaka mmoja. Hali hii imeonesha uwekaji wa mikakati kwamba uchumi wa China umeanza kupata maendeleo kwa kiwango cha juu, na kuhimiza utekelezaji wa mageuzi katika sekta mbalimbali.

    Hali nyingine inayofuatiliwa na watu ni kwamba, katika ripoti hiyo nchi mbili za Afrika, za Mauritius na Rwanda, zimezidi nafasi za China na Japan kwa kushika nafasi za 20 na 29, hali ambayo imeonesha kuwa, ripoti hiyo ilitolewa kwa kufanya tathmini bila ya kujali ukubwa wa kundi la uchumi, na inazingatia zaidi utekelezjiutekelezaji wa hatua halisi za mageuzi.

    Tangu mwaka huu, rais Xi Jinping wa China imesisitiza kwa mara nyingi kwamba, China itaweka mkazo mkubwa katika kuboresha mazingira ya biashara nchini China. Kwenye Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China yaliyofunguliwa jana, rais Xi ameweka "Kujenga mazingira ya biashara ya kimataifa yawe kiwango cha juu duniani" kama kipaumbele katika mchakato wa ufunguaji mlango. Akisisitiza kuwa China itaheshimu mazingira ya biashara ya kimataifa, na kuviyatendea kwa usawa viwanda vyote vilivyosajiliwa nchini China, pia itaadhibu vitendo vyote vya kuharibu haki halali ya wafanyabiashara wa kigeni, pamoja na vile vinavyokiuka hakimiliki ya ujuzielimu.

    Kadiri idara mbalimbali za serikali za China zinavyotangaza sera na hatua za kuunga mkono maendeleo ya uchumi wa sekta ya binafsi nchini China, haswa hadi hatua za mageuzi ya mashirika ya China zitakapotekelezwa kwa pande zote mwishoni mwa mwaka huu, ndivyo mazingira ya biashara yatakuwa wazi, ywenye uvumbuzi na uvumilivu zaidi, na yatachangia zaidi ufunguaji mlango wa China kufika kwenye kiwango cha juu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako