• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Uchumi mwaimarika kwa miaka mmitatu ya uongozi wa Magufuli

  (GMT+08:00) 2018-11-06 17:34:16

  Ni miaka mitatu tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dk John Magufuli amefanya mambo kadhaa ili kuhakikisha nchi inafikia malengo yake ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo 2025. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi alipokuwa akitoa taarifa ya mambo muhimu yaliyotekelezwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli tangu alipoanza kutawala hadi sasa.

  Katika mwaka 2017/18 uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia 7.1 na kuifanya kuwa ya kwanza kwa Afrika Mashariki lakini katika takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB) ni ya Tisa kati ya nchi 10 duniani ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi.

  Akiyataja mashirika ambayo yalikuwa yakipigiwa kelele na kuonekana kuwa ni mzigo kwa maendeleo ya Taifa lakini ndani ya miaka mitatu ya ufuatiliaji wake Rais Magufuli ameweza kuyafufua ni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Reli (TRC), Mamlaka ya maji safi na maji taka Dar es Salaam (DAWASA) na Mamlaka ya Bandari (TPA). Rais Magufuli alipoingia katika madaraka aliahidi kujenga viwanda ambapo ndani ya miaka mitatu jumla ya viwanda 3306 vimeandikishwa, vinaendelea kujengwa na baadhi vimekamilika na vinatoa bidhaa mbalimbali, kati ya hivyo 251 ni vikubwa na 173 ni vya kati.

  Aidha Dk Abbasi amewaasa Watanzania kuendeleza utamaduni wa kulipa kodi ili fedha hizo zikatumike kukamilisha miradi ya maendeleo muhimu kwa taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako