• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mbona uzalishaji wa pamba ukadorora

    (GMT+08:00) 2018-11-06 17:34:48

    Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Marco Mtunga amewaeleza wadau wa pamba sababu kuu tatu zilizosababisha kushindwa kufikia malengo ya kuzalisha pamba msimu wa mwaka 2017/18. Mtunga alizitaja sababu hizo kuwa ni ukame mkali uliotokea kati ya Januari na Februari ambao ulipukutisha vitumba vichanga na mvua kubwa kupita kiasi kati ya Machi na Mei, iliyozamisha pamba maeneo yote ya mbuga na mabondeni.

    Sababu nyingine ambayo imeonekana kuwa kubwa zaidi ni mlipuko wa wadudu wakiwamo viwavi jeshi, vindung'ata, chawajani, vithiripi, vidukari na wadudu wanaofyonza ambao hawakuwepo miaka iliyopita.

    Mtunga alisema hayo kwenye mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya pamba uliofanyika jijini Mwanza, mwenyekiti wake akiwa Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba.

    Mtunga alisema walilenga kuzalisha tani 500,000 za pamba lakini walizalisha tani 200,000 sawa na asilimia 67 kwa mikoa 17 inayolima zao hilo.

    Alisema kwa msimu huo zilisambazwa mbegu tani 18,500, viuadudu lita 5.9 milioni na vinyunyizi 23,500.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako