• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima wapinga bei mpya ya mahindi iliyotangazwa na serikali

    (GMT+08:00) 2018-11-06 17:35:14

    Baada ya serikali ya Kenya kutangaza kuwa gunia moja la mahindi ya kilo 90 kununuliwa kwa shilingi 2,300, wakulima wa mahindi na wasagaji nafaka wamejitokeza na kupinga bei hii mpya. Serikali ilitangaza bei hii mpya kwa na kuahidi kununua magunia milioni 2.5 ya mahindi msimu huu wa mavuno.

    Wakulima wanasema bei ya Sh2,300 kwa gunia moja la kilo 90 ni hasara kwao kwani hawataweza kurejesha gharama waliyotumia katika uzalishaji wa mahindi.

    Vilevile, wanasema kuwa hatua ya serikali kupunguza bei hiyo itasabababisha baadhi yao kuuza zao lao kwa wafanyabiashara .

    Bei hiyo mpya ambayo ilitangazwa na Bodi ya Hazina ya Hifadhi ya Chakula Nchini, Strategic Food Reserve Trust Fund (SFRTF) ni ya chini kuliko bei ya mwaka2017 ya Sh3,200 kwa gunia la kilo 90.

    Nao wasagaji wanasema kuwa bei hiyo mpya itachangia kupanda kwa bei ya unga kuzidi Sh75 kwa paketi ya kilo mbili iliyotangazwa na serikali Oktoba 2018.

    Wanasema hali hii itachangia kupanda kwa bei ya unga hadi Sh85 au Sh90 kwa paketi ya kilo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako