• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ndondi kufutwa michuano ya Olimpiki

  (GMT+08:00) 2018-11-07 09:07:43
  Chama cha kimataifa cha ndondi (AIBA) kiko hatarini kufungiwa na kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC) kufuatia uamuzi wake wa kumchagua Gafur Rakhimov kuwa rais wao wa kudumu katika mkutano uliofanyika nchini Uswisi.

  Ujumbe wa AIBA umepuuza onyo toka IOC ambalo linapinga kumchagua mtu ambaye wamemuelezea kuwa ni mmoja wa waharifu wanaoongoza nchini Uzbekistan.

  OIC imeweka wazi changamoto za AIBA kuhusu uamuzi, fedha, masuala ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni ambazo zimepigwa marufuku pamoja na utawala bora.

  Rakhimov yupo katika orodha iliyotolewa na idara ya fedha ya Marekani ya watu waliopigwa marufuku kujihusisha na michezo kutokana na shutuma ya usafirishaji wa kimataifa wa dawa za kulevya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako