• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji

    (GMT+08:00) 2018-11-07 12:06:27

    Kongamano kuhusu uwekezaji nchini Afrika Kusini limefanyika jana mjini Shanghai, China. Waziri wa biashara na viwanda wa Afrika Kusini Bw. Rob Davis amesema Afrika Kusini inatumai kupitia kongamano hilo kuonyesha kwa pande zote sura ya taifa ya Afrika Kusini na uwezekano wa uwekezaji, na inatumai kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji ili kutoa urahisi zaidi kwa kampuni na wawekezaji wa China. Amesema :

    "Rais Cyril Ramaphosa ametangaza mpango wa kuvutia uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 100 ndani ya miaka mitano ijayo. Tuna imani kupitia kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji kutimiza lengo hilo, na kuleta maendeleo ya kasi zaidi ya uchumi wa Afrika Kusini, ili kukabiliana changamoto tulizokabiliwa nazo katika kujiendeleza."

    Bw. Rob Davis pia amesema, baada ya kuongezeka kwa ushirikiano na biashara kati ya China na Afrika Kusini, mustakabali wa uwekezaji wa China nchini Afrika Kusini utakuwa mzuri zaidi.

    Mwenyekiti wa CPPCC akutana na ujumbe wa muungano wa baraza la uchumi na jamii wa Afrika

    Mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China CPPCC Bw. Wang Yang, jana hapa Beijing alikutana na ujumbe wa muungano wa baraza la uchumi na jamii wa Afrika, unaoongozwa na mwenyekiti wake ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la uchumi na jamii la Mali Bw. Boulkassoum Haiara.

    Bw. Wang Yang amesema mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika mwezi Septemba mwaka huu, na kuongoza uhusiano kati ya pande hizo mbili kuingia katika kipindi kipya. Amesema China itaendelea kufuata wazo la rais Xi Jinping wa China na kushirikiana na Afrika kuhimiza ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kati ya pande mbili kuharakisha utekelezaji wa matokeo ya mkutano huo, na kuimarisha zaidi msingi wa kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa China na Afrika.

    Bw. Haiara amesema, anatumai kufanya umuhimu wa baraza la uchumi na jamii, kufanya juhudi kwa ajili ya kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana katika pande mbalimbali, na kuzidisha uhusiano kati ya Afrika na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako