• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Boeing kuleta ndege ya 2000 nchini China

    (GMT+08:00) 2018-11-07 16:58:32

    Shirika la kutengeneza ndege la Marekani Boeing limesema, litaleta ndege yake ya 2000 nchini China ndani ya mwaka huu.

    Kaimu rais wa kampuni hiyo kanda ya Asia Kaskazini Mashariki Bw. Rick Anderson amesema hayo katika maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya China ya Safari za Anga na Anga za Juu yanayofanyika Zhuhai, mkoani Guangdong hapa China. Amesema Boeing imewasilisha ndege 153 kwa kampuni za ndege za China katika robo tatu za mwanzo za mwaka huu, na kwamba idadi ya ndege zilizoletwa nchini China inapita 140 katika miaka 6 iliyopita.

    China iliagiza ndege 10 aina ya Boeing mwaka 1972, na kuwa mwanzo wa uwepo wa kampuni hiyo nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako