• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar yakumbwa na uhaba wa mchele

    (GMT+08:00) 2018-11-07 18:48:17

    Zanzibar imekumbwa na uhaba wa mchele aina ya mapembe ambao hutumiwa sana na wananchi wenye kipato cha chini.

    Uhaba huo umejitokeza wakati ambapo kuna uhaba wa mafuta aina ya petrol na dizeli visiwani Zanzibar.

    Kutokana na hali hiyo,bei ya mchele huo sasa impenda Sh,1,500 kutoka Sh1,300 kwa kilo moja.

    Waziri wa Biashara na Viwanda,Balozi Amina Salum Ali,alisema katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Zanzibar kwamba ongezeko la bei limetokana na kuadimika kwa mchele huo katika soko la dunia.

    Alisema licha ya changamoto hizo,zaidi ya makontena 200 ya mchele huo yameshawasili Zanzibar na pia waagizaji wengine wanatarajia kuingiza hivi karibuni,na hivyo bei itashuka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako