• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bei ya bidhaa za petroli yaongezeka Rwanda

  (GMT+08:00) 2018-11-07 18:48:58
  Bei za bidhaa za petroli,ambazo ziliongezeka wiki hii,hazitaathiri nauli ya usafiri wa umma kwa sababu bado zinasalia katika viwango vya sasa vya nauli ya usafiri wa umma.

  Mkurugenzi wa Udhibiti wa Uchumi katika Mamlaka ya Udhibiti ya Rwanda,Dkt Benjamin Rutimirwa,jumanne alisema bei za mafuta nchini humo zimeongezeka kwa sababu vipengele vikuu vitatu ambavyo vinaongeza bei ya mafuta,pia vimeongezeka.

  Alisema kuwa nchini Rwanda,bei ya bidhaa za petroli inasukumwa na bei katika soko la kimataifa,viwango vya ubadilishanaji wa fedha za kigeni,gharama za usafirishaji kutoka nchi za uagizaji hadi Kenya na Tanzania ambako Rwanda inachukua bidhaa zake za petroli.

  Bei mpya za mafuta zimeanza kutekelezwa leo jumatano huku dizeli ikiuzwa Rwf1,148 kwa lita kutoka Rwf1,093.

  Petroli inauzwa Rwf1,132 kwa lita kutoka Rwf1,109.

  Mabadiliko hayo yanawakilisha ongezeko la Rwf55 na Rwf23 kwa dizeli na petroli.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako