• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • FKF yaipigia magoti serikali yaomba milioni 83

  (GMT+08:00) 2018-11-08 08:44:36
  Timu zote za taifa nchini Kenya zipo kwenye wakati mgumu kiuchumi na kupelekea hatihati ya kushiriki mashindano yanayozikabili. Timu ya taifa ya wanaume Harambee Stars, timu ya taifa ya wanawake Harambee Starlets na za wadogo Emerging Stars.

  Rais wa FKF Nick Mwenda amesema zinahitajika milioni 83 vinginevyo Kenya inaweza kusahau ushiriki wake kwa sasa. Harambee stars inajiandaa kwa mchezo wa Novemba 18 utakaopigwa katika uwanja wa Moi Kasarani kusaka tiketi ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2019), huku kikosi cha wanawake Harambee Starlets kinatarajiwa kuondoka Novemba 14 kuelekea Accra Ghana kushiriki michuano ya AWCON, na timu ya vijana u23 wao wanajiandaa kukipiga na Mauritius Novemba 14 kusaka tiketi kwenda fainali za AFCON U23 zitakazofanyika mwakani nchini Misri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako