• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yaeleza hali ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kufanya mapitio kuhusu China

    (GMT+08:00) 2018-11-08 09:45:19

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying ameeleza hali ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kufanya mapitio kwa duru ya tatu kuhusu hali ya haki za binadamu nchini China.

    Bibi Hua Chunying amesema ujumbe wa China umeeleza mafanikio makubwa iliyopata China katika sekta za haki za binadamu tangu mapitio ya duru iliyopita ya mwaka 2013, kueleza njia ya kujiendeleza na mtazamo kuhusu haki za binadamu wenye umaalumu wa China, mwelekeo wa maendeleo ya kuhakikisha na kuhimiza haki za binadamu, na kutangaza hatua mpya 30 za kuhakikisha haki za binadamu zitakazochukuliwa na China.

    Bibi Hua Chunying amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kuimarisha maingiliano na kufundishana, ili kupata maendeleo kwa pamoja kwa msingi wa kuwa na usawa na kuheshimiana, kusikiliza kwa makini na kupokea maoni ya dhati na ya kiujenzi. Pia amesema China inapinga kithabiti na kukataa lawama za baadhi ya watu wenye maoni ya upande mmoja ya kisiasa na bila msingi wowote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako