• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Majeshi ya serikali na waasi nchini Sudan Kusini wafanya mkutano wa kwanza wa kuimarisha amani

  (GMT+08:00) 2018-11-08 09:48:09

  Jeshi la serikali ya Sudan na kundi kuu la waasi linaloongozwa na aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais wa nchi hiyo Bw.Riek Machar yamefikia makubaliano muhimu kuhusu kusimamisha uhasama na kuruhusu upatikanaji wa misaada ya kibinadamu bila vizuizi.

  Msemaji wa jeshi la serikali Bw. Lul Ruai Koang amesema wameafikiana na viongozi wa waasi kuwapa wapiganaji uhuru wa kuhama, kuimarisha usalama wa raia na kutozuia misaada ya kibinadamu.

  Mkutano huu kati ya pande hizo mbili umefanyika baada ya rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Bw. Machar kusaini makubaliano ya kumaliza vita iliyodumu kwa miaka minne. Kutokana na makubaliano hayo, Bw. Machar atarudi mjini Juba mwezi Mei mwakani, na kuchukua tena nafasi ya makamu wa kwanza wa rais wa nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako