• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Russia yasema kuna dalili za ushirikiano kati ya kundi la IS na kundi la Al-Qaeda

  (GMT+08:00) 2018-11-08 16:30:56

  Mkurugenzi wa Idara ya usalama ya Russia Bw. Alexander Vasilevich Bortnikov jana huko Moscow amesema, dalili mfululizo zinaonesha kuwa kundi la IS na kundi la Al-Qaeda zinafanya ushirikiano kwa siri.

  Bw. Bortnikov amesema, Russia inashuku makundi hayo yanatumia mtandao wa pamoja, na kueneza mawazo ya kidini yenye siasa kali kwa njia ya matangazo ya pamoja. Licha ya hayo, makundi hayo pia yanatumia wanachama wao kuunga mkono upande mwingine.

  Bw. Bortnikov amesema, kwenye baadhi ya kesi, makundi ya IS na Al-Qaeda yalipata fedha, zana na rasilimali ya ufundi kwa njia ya pamoja na kutoka mwanzo mmoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako