• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonesho ya CIIE yafungua zama mpya ya "ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi"

  (GMT+08:00) 2018-11-08 18:52:46

  Zaidi ya aina 100 za teknolojia na bidhaa zimeoneshwa katika Maonesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China CIIE yanayoendelea mjini Shanghai. Mashirika ya utafiti, pamoja na wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali wameleta bidhaa zao za teknolojia za kisasa kwenye maonesho hayo. Wanachozingatia si kama tu ni soko kubwa la China, bali pia juhudi kubwa za China zilizofanyika katika kulinda hakimiliki ya ujuzi katika miaka mingi iliyopita.

  Hivi sasa China imeingia katika nafasi 20 za mwanzo kwa kufuata vigezo ya uvumbuzi duniani vilivyotolewa na Shirika la hakimiliki ya ujuzi la dunia mwaka 2018, na uvumbuzi umekuwa msukumo muhimu wa China katika kupata maendeleo yenye kiwango cha juu. Bw. Bill Gates anayeshiriki kwenye baraza la uchumi na biashara la kimataifa ameeleza kuwa, matokeo mengi ya uvumbuzi si kama tu ni ya kujinufaisha, bali pia yanaihudumia dunia.

  Jambo linalofuatiliwa zaidi na wafanyabiashara wanaoshiriki kwenye maonesho hayo ni hotuba aliyoitoa rais Xi Jinping wa China. Rais Xi ameahidi kujenga mazingira yenye kiwango cha juu cha biashara, hatua halisi ni pamoja na "Kuadhibu vikali vitendo vya kukiuka haki halali ya wafanyabiashara wageni, hususan vitendo vinavyokiuka hakimiliki ya ujuzi, na kuinua ubora na ufanisi wa kufanya ukaguzi kuhusu hakimiliki ya ujuzi, hatua ambazo zitalinda vizuri matokeo ya ubunifu ya dunia, na kuwafanya wafanyabiashara wageni kuwekeza, kufanya utafiti na kutumia teknolojia bila wasiwasi, na kunufaika na maendeleo yaliyopatikana nchini China.

  Likiwa baraza kuu la hakimiliki ya ujuzi lililofanyika kwenye Maonesho ya CIIE, mkutano wa ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi na uendelezaji wa uvumbuzi duniani uliofanyika tarehe 6, vilevile umehusisha mashirika ya kimataifa, maofisa, wataalamu na wasomi pamoja na wajumbe wa serikali kutoka nchi na sehemu zaidi ya 20 duniani, wakijadiliana kwa kina kuhusu mada ya ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi, kuhimiza maendeleo ya uvumbuzi, na kujenga mazingira ya kiwango cha juu ya biashara, na kutoa mapendekezo kwa ajili ya mkondo wa uvumbuzi duniani. Hali ambayo pia imeonesha uwajibikaji wa majukumu ya China katika kulinda hakimiliki ya ujuzi duniani. Kama rais Xi Jinping alivyosema, nchi zote zinatakiwa kuboresha mazingira ya biashara, kutatua masuala yaliyokuwepo ndani yake, badala ya kujipamba huku ikilaumu wengine. Hivi sasa Maonesho ya CIIE yanayoendelea yamefungua zama mpya kwa ulinzi wa hakimiliki duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako