• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda yatarajia kuwa na huduma bora za afya kwa wakina mama na watoto ifikapo mwaka 2024

  (GMT+08:00) 2018-11-08 19:17:25

  Waziri wa afya wa Rwanda Bi. Diane Gashumba amesema, nchi hiyo inatarajia kuwa na huduma bora ya afya kwa wakina mama, wajawazito na watoto ifikapo mwaka 2024.

  Akizungumza kwenye mkutano wa siku tatu wa huduma ya Dharura ya Afya ulioanza jana mjini Kigali, Rwanda, Bi. Gashumba amesema serikali ya nchi hiyo itaongeza vituo vya afya katika kila tarafa nchini humo ili kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa huduma za afya.

  Mkutano huo umekutanisha washiriki 500 wakiwemo madaktari, wauguzi, wasaidizi wa madaktari, wabunge na maofisa wa serikali pamoja na wadau kutoka nchi 45 duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako