• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima wa pamba wanufaika na matrekta kutoika Benki ya Maendeleo ya Kilimo

  (GMT+08:00) 2018-11-08 19:37:05

  Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini Tanzania (TADB),imetoa matrekta 50 yenye thamani ya zaidi ya Sh2.7 bn kwa vyama vya ushirika 50 (AMCOS) vinavyolima pamba katika mikoa ya kanda ya Ziwa ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Kamimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,Japhet Justine,amesema TADB inalenga kuwawezessha wakulima wa zao la pamba nchini Tanzania ili kuongeza tija na uzalishaji kama inavyobainishwa katika Mpango wa Maendeleo ya kilimo Awamu ya Pili (ASDP-11).

  Alisema matrekta ni sehemu ya utekelezaji wa ASDP-11 katika kuhakikisha nyenzo bora za kilimo zinawafikia wakulima na kuchagiza uzalishaji zaidi wa malighafi zitakazotumika kwenye viwanda na kufanikisha azma ya serikali ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako