• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanawake 15 kupata ufadhili wa pesa kusaidia miradi yao Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-11-08 19:39:22
    Wanawake 15 walio na miradi bora ya biashara nchini Rwanda watapigwa jeki ya pesa taslimu kati ya $5,00, na $10,000 kuboresha biashara zao.

    Hii ni sehemu ya 'Wiki ya Wajasiriamali Ulimwenguni' ambayo itawaleta pamoja wajasiriamali zaidi ya 4,000 haswa vijana na wanawake,kujadiliana jinsi watakavyoweza kuboresha biashara zao.

    Pia inalenga kujadili changamoto zinazowaathiri wajasiriamali wanawake ,upatikanaji wa fedha ,miongoni mwa mambo mengine.

    Kulingana na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la serikali la IDEA4Africa nchini Rwanda Bi Pamela Munyana, ambao wanaandaa tkuio hilo la wiki ya wajasiriamali,wiki hii inalenga kuwainua wanawake walio na miradi mizuri.

    Alisema kwamba wanawake watachaguliwa wikendi hii na kuongeza kuwa shirika lake pamoja na washirika wengine wametafuta pesa za kusaidia miradi ya wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako