• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vijana waanza ufugaji kuku Murang'a Kenya

  (GMT+08:00) 2018-11-08 19:39:42

  Baadhi ya vijana katika Kaunti ya Murang'a nchini Kenya wameachana na biashara ya uchukuzi wa bodaboda na kuanza biashara ya ufugaji kuku.

  Vijana hao wamemuandikia barua Gavana wa kaunti hiyo Mwangi wa Iria wakiitaka serikali yake iwatengee Sh30 milioni kwa ajili ya miradi ya ufugaji huo.

  Vijana hao wanasema kuwa kila mhisani akitaka kuwasaidia huwanunulia bodaboda,lakini wameona kuwa biashara hiyo ya uchukuzi haina tija kama biashara ya ufugaji kuku.

  Mwenyekiti wa muungano wa vijana wawekezaji katika kaunti hiyo,Martin Mwau amesema takwimu zake

  zinaonyesha kuwa licha ya wingi wa bodaboda katika mitaa ya kaunti hiyo, kiwango cha ukosefu wa ajira kimesimamia asilimia 38 ya vijana.

  Aidha anasema kuwa kinyume na bodaboda, kundi la ufugaji kuku lina uwezo wa kuanza kuvuna faida nono katika mwezi wa nne.

  Mwau anasema kuwa hesabu hii ya kuku huwa na utamu wa pato kwa kuwa ukiwa na kuku hao wa kutaga mayai 120 ina maana kuwa pato limegonga Sh30,000 kwa mwezi, pesa ambazo ndio mshahara wa wengi wa waajiriwa wa serikali na pia katika sekta binafsi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako