• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Muungano wa Ulaya kufadhili ujenzi wa viwanda vinne

  (GMT+08:00) 2018-11-08 19:40:02
  Muungano wa Ulaya,(EU) umetia saini mkataba wa kufadhili ujenzi wa viwanda vine vyenye mitambo ya kuhifadhi maziwa katika maeneo ya Tana Kaskazini na Tana Delta.

  Mitambo hiyo itawekwa ndani ya miaka miwili,na inanuiwa kuniua uchumi katika kaunti ya Tana River ,na kuongeza mapato kwa wafugaji wa ng'ombe na maziwa.

  Mkurugenzi wa Idara ya Mifugo,Bw Nzioka Wambua amesema mradi huo utasaidia kupunguza uharibifu ambao wafugaji wamekuwa wakishuhudia kwa muda sasa kwa maziwa kuharibika na pia kuimarisha uzalishaji tofauti na hapo awali ambapo wakulima walipata hasara kubwa.

  Wambua alisema miradi hiyo itawekwa katika maeneo ya Bangale,Boka,Garsen na Odha,huku wanaolengwa wakiwa wafugaji wanaoishi au kulisha mifugo katika sehemu hizo.

  Katika maeneo ya Bangale na Boka, mitambo hiyo itatumika katika ukusanyaji wa maziwa kutoka kwa wafugaji,kuhifadhi kwa majokofu,na kuyatayarisha na kuweka kwa pakiti kabla ya kusafirisha maziwa hayo kwa masoko ya Garissa na Nairobi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako