• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Henry Kissinger

    (GMT+08:00) 2018-11-08 20:20:36

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Henry Kissinger.

    Kwenye mazungumzo yao, rais Xi amesema hivi karibuni lawama za Marekani dhidi ya China zimeongezeka, hali inayotakiwa kufuatiliwa. Pia amesisitiza kuwa China inashikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, na inapenda kutatua ipasavyo matatizo yaliyopo kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa njia ya majadiliano ya kirafiki. Wakati huo huo Marekani inapaswa kuheshimu haki ya China ya kujiendeleza kwa njia zinazochaguliwa nayo, na kulinda kwa pamoja uhusiano kati ya pande hizo mbili kupata maendeleo kwa hatua madhubuti.

    Naye Bw. Kissinger amesema, Marekani na China zinahitaji kuelewana vizuri zaidi, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kupanua maslahi ya pamoja, na kudhibiti migongano iliyopo kati yao, na kuonesha dunia kwamba maslahi ya pamoja kati ya pande hizo mbili ni kubwa zaidi kuliko mikwaruzano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako