• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA WANAWAKE: FKF yasikitishwa na hatua ya CAF kuhusu timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya

  (GMT+08:00) 2018-11-09 08:43:35
  Shirikisho la soka nchini Kenya, limesikitishwa na hatua ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF, kubadilisha uamuzi wa awali wa timu ya taifa ya soka ya wanawake, Harambee Starlets kushiriki katika mashindano ya bara Afrika inayoanza tarehe 17 mwezi huu nchini Ghana.

  Kenya ilikuwa imeruhusiwa kushiriki katika mashindano hayo, baada ya kuondolewa kwa Equitorial Guinea iliyopatikana na kosa la kumchezesha mchezaji wa taifa lingine katika timu yake ya taifa.

  Hata hivyo, Equitorial Guinea ilikata rufaa ikisisitiza kuwa mchezaji huyo ni raia wa nchi hiyo , rufaa ambayo imezaa matunda na CAF kukubaliana nayo na kuirejesha timu hiyo kwenye mashindano hayo na kuiondoa Kenya.

  Rais wa FKF, Nick Mwendwa, ameiandikia barua na kutaka kuahirisha mashindano hayo au yaendelee lakini yaruhusiwe kuwa na mataifa tisa yatakayoshiriki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako