• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UEFA yapanga muda wa kutambulisha VAR, msimu huu

  (GMT+08:00) 2018-11-09 08:44:35
  Mfumo wa usaidizi wa video (VAR) unaweza kutambulishwa kwa haraka katika hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa ya msimu huu, shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limesema limeamua kufanya uamuzi kwa mwezi ujao.

  Shirikisho hilo linaloongoza soka barani Ulaya lilisema mnamo Septemba kuwa VAR itaanzishwa kuanzia msimu wa 2019/20, lakini majadiliano yameendelea kwa wiki kadhaa za hivi karibuni, na kuonyesha nia ya kutambulishwa haraka zaidi mfumo huo tofauti na ilivyotegemewa.

  hofu ya UEFA kutokana na makosa ya waamuzi katika michezo mbalimbali na mafanikio ya VAR katika Kombe la Dunia mwaka huu, ni moja ya vishawishi vikubwa kwa viongozi hao kufikiria upya suala la kutambulisha teknolojia hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako