• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Zambia asema CIIE ni fursa nzuri kwa makampuni ya nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2018-11-09 09:36:09

    Balozi wa Zambia nchini China bibi Winnie Natala Chibesakunda amesema, maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China CIIE ni fursa nzuri kwa makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati ya Zambia, na yatatoa mchango kwa maendeleo ya viwanda nchini Zambia. Bibi Chibesakunda anasema,

    "Makampuni mengi madogo na ya ukubwa wa kati yanashiriki kwenye maonesho ya CIIE, na kuleta matoleo yao. Makampuni hayo yamefurahia kupata oda nyingi. Naamini kuwa baada ya kurudi Zambia, yatainua kiwango chao cha uzalishaji kwa kutumia fedha yalizopata. Hii ni sehemu ya juhudi za kuhimiza maendeleo ya viwanda barani Afrika kutokana na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika. China imefungua zaidi soko lake kwa makampuni ya Zambia, na itasaidia nchi yetu kuinua kiwango cha biashara ya kimataifa na viwanda."

    Kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Beijing mwaka huu, rais Xi Jinping wa China alieleza kuunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye maonesho ya CIIE kwa kusamehe ada za ushiriki. Bibi Chibesakunda anasema,

    "Rais Xi hutimiza ahadi zake kila mara. Serikali ya China imeyasaidia makampuni yetu kwa pande zote. Serikali ya Zambia inafurahi na kuishukuru China kwa kutupa fursa ya kushiriki kwenye maonesho haya. Bila msaada wa China tusingekuwa na fursa nzuri ya kujiendeleza."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako