• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bill Gates asema ujenzi wa mambo ya digitali wa China umeendelezwa kwa kasi zaidi duniani

    (GMT+08:00) 2018-11-09 09:43:03

    Mwenyekiti mwenza wa Shirika la The Bill & Melinda Gates la Marekani Bw Bill Gates amesema China imepata maendeleo ya kasi na kufanya uvumbuzi kwenye sekta nyingi, na ujenzi wa mambo ya digitali wa China umeendelezwa kwa kasi zaidi duniani.

    Amesema hivi sasa watu wengi zaidi wa China wamezoea kulipa kwa kutumia njia ya kidigitali, kama vile mtandao wa internet au simu ya mkononi. Shirika lake litasaidia nchi maskini katika kuendeleza sekta ya fedha inayotumia teknolojia ya digitali.

    Ameongeza kuwa Maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje (CIIE) yanaonyesha kwamba China inatoa mchango wa kurekebisha mazingira ya soko la biashara, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha ushindani na kuvutia mitaji kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako