• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lasifiwa kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Uchukuzi wa Barabarani

    (GMT+08:00) 2018-11-09 16:19:58

    Mkutano wa kimataifa wa uchukuzi wa barabarani umefungwa tarehe 8 huko Muscat, mji mkuu wa Oman, huku pendekezo la China la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" likisifiwa na washiriki.

    Mktuano huo wa siku tatu uliowashirikisha wajumbe kutoka nchi na sehemu zaidi ya 70 duniani, umefikia "makubaliano ya Muscat", ukizihimiza idara na mashirika yanayoshughulikia uchukuzi duniani kuchukua hatua kwa pamoja, kuimarisha ushirikiano na kuzidisha uelewa katika sekta nne zikiwemo kuwaandaa wataalamu, kupanua mawasiliano ya kibiashara, kulinda mazingira na kuongeza nguvu katika uvumbuzi.

    Mshiriki wa mkutano huo ambaye alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jose Manuel Barroso amesema, maendeleo ya China yametoa mfano mzuri kwa dunia nzima, na pendekezo la China la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limeunganisha biashara ya dunia nzima, hali inayosaidia kupunguza vizuizi kati ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako