• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya CIIE yafungua mlango mpya kwa nchi zinazoendelea

    (GMT+08:00) 2018-11-10 18:19:55

    Kwenye Maonesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Uingizaji Bidhaa ya China CIIE, wafanyabiashara kutoka nchi zinazoendelea na nchi zilizoko nyuma kimaendeleo wameleta bidhaa zao, na kuvutia waagizaji wengi kufanya ushirikiano.

    Wakati nchi zilizoendelea zinapoonyesha matoleo yao ya teknolojia ya juu, nchi zinazoendelea na nchi zilizoko nyuma kimaendeleo pia zimeleta bidhaa zao zenye umaalumu wao, zikiwemo vyakula, bidhaa za kilimo, nguo, bidhaa za matumizi ya kila siku pamoja na rasilimali ya utalii na utamaduni wao.

    Watu wanaona kwamba, kujipatia maisha mazuri ni matumaini ya pamoja ya watu wa kila nchi. Wazo la "jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja" na pendekezo la "kushikilia ushirikiano shirikishi na wa kunufaishana, na kuhimiza nchi mbalimbali kujiendeleza kwa pamoja" yaliyotolewa na rais Xi Jinping wa China kwenye ufunguzi wa maonyesho ya CIIE yameelekeza njia sahihi ya kutimiza matumaini hayo.

    Kutokana na juhudi za pamoja za China na nchi mbalimbali, maonyesho ya CIIE yamekuwa jukwaa la kunufaikha na utandawazi wa kimataifa. Nchi zinazoendelea na nchi zilizoko nyuma kimaendeleo zimepata fursa na soko kwenye maonyesho hayo. Mkurugenzi mkuu wa WTO Bw. Roberto Azevedo amesema kuwa, kwa muda mrefu China na nchi zinazoendelea zikiwemo nchi zilizoko nyuma kimaendeleo zimejenga uhusiano mzuri, na China kupanua uingizaji wa bidhaa kutoka nje kutanufaisha nchi hizo.

    Kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa, na kukabiliana na hatari na changamoto zinazowakabili binadamu wote, juhudi ya China tu haitoshi, inahitaji nchi mbalimbali duniani kuondoa tofauti na kuhimiza maendeleo shirikishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako