• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuweka mazingira mazuri zaidi ya kuhimiza uchumi binafsi

    (GMT+08:00) 2018-11-11 17:50:43

    Naibu mkuu wa Kamati ya maendeleo ya mageuzi China, ambaye pia ni mkuu wa idara ya takwimu ya China Bw. Ning Jizhe, amesema China itatoa fursa nyingi zaidi za uwekezaji na huduma nzuri zaidi kwa biashara binafsi. Amesema China itahimiza miradi mbalimbali kwenye sekta za usafiri, nishati, mazingira na ulinzi wa mazingira, kuendana na sera za viwanda za taifa, huku kukiwa na maandalizi ya kutosha na utaratibu ulio wazi wa biashara hizo kupata faida.

    Kila mwaka China itachapisha orodha ya miradi inayotangazwa kwa biashara binafsi, ikifuatiwa na uungaji mkono na huduma.

    Bw. Jizhe amesema tayari China imetekeleza miradi ya majaribio ya umiliki wa ubia kwenye sekta za umeme, mafuta, gesi, reli, mambo ya anga, mawasiliano ya simu na viwanda vya kijeshi. Pia amesema China italinda haki miliki ya biashara binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako