• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CAF yatoa ratiba ya michezo ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa na Shirikisho barani Afrika.

  (GMT+08:00) 2018-11-12 09:08:44
  Shirikisho la soka Afrika CAF leo limepanga ratiba ya michezo ya kwanza ya michuano ya ligi klabu bingwa barani Afrika (CAF Champions League) na michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, ambapo Tanzania inawakilishwa na Simba na Mtibwa Sugar.

  Samba itaanza kukipiga na Mbabane Swallows ya Swazi katika mchezo utakaochezwa kati ya Novemba 27 na 28 jijini Dar es salaam, mshindi wa jumla wa mechi hizo atakutana na Nkana Red Devils ya Zambia na UD Do Songo ya Msumbiji ili kusaka timu itakayofuzu hatua ya makundi.

  JKU ya Zanzibar itaanzia nyumbani itakapokutana na Al Hilal ya Sudan na mshindi wa jumla atakutana na APR ya Rwanda na Club Africains ya Tusinia.

  Kwenye kombe la shirikisho, Mtibwa Sugar ya Tanzania imepangwa kukutana na Northern Dynamo ya Shelisheli na mshindi wa mechi hiyo atakutana na KCCA ya Uganda wakati Zimanimoto ya Zanzibar itaanza na Kaizer Chief ya Afrika Kusini na ikishinda game hii itakutana na kati ya El Geco ya Madagascar ama Deportivo Unidado ya Equitor Guinea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako