• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya sheria ya China yatoa waraka ili kuweka mazingira mazuri ya kisheria kwa ajili ya maendeleo ya viwanda vya binafsi

    (GMT+08:00) 2018-11-12 16:42:49

    Wizara ya sheria ya China hivi karibuni imetoa waraka unaozitaka idara za ngazi mbalimbali za utekelezaji wa sheria kufanya kazi ya kuweka mazingira mazuri ya kisheria kwa ajili ya maendeleo ya viwanda binafsi. Waziri wa sheria wa China Bw. Fu Zhenghua amesema, wizara yake itasukuma mbele kukamilisha sheria za kuhimiza maendeleo ya uchumi binafsi, ili kuweka uhakikisho thabiti wa kisheria kwa ajili ya maendeleo ya viwanda binafsi.

    Ili kuunga mkono na kuhimiza maendeleo ya viwanda binafsi, kuweka mazingira ya kisheria ya kufanya biashara yaliyo ya haki na wazi zaidi, wizara ya sheria ya China hivi karibuni imetangaza waraka kuhusu kufanya kazi kutosha ili kuweka mazingira mazuri ya kisheria kwa ajili ya maendeleo ya viwanda binafsi. Waziri wa sheria wa China Bw. Fu Zhenghua amesema kuwa,

    "Wakati tulipoandaa waraka huo, tuliacha ulinzi mtupu. Mara hii tumesisitiza kanuni ya kuruhusu viwanda binafsi kuingia katika sekta zisizowekwa vizuizi na sheria. Huo ni ulinzi halisi kwa uchumi binafsi, na ulinzi wenye nguvu."

    Habari zinasema waraka huo umeharakisha mchakato wa kutunga, kurekebisha, kuondoa na kufafanua sheria husika, kuhusu masuala halisi yaliyovikumba na viwanda binafsi katika udhibiti wa kuingia kwenye soko, ulinzi wa hakimiliki, uwekezaji na kuvutia mitaji, ushindani wenye haki n.k..

    "wizara ya sheria ya China imeziagiza idara mbalimbali za sheria kote nchini, kupitia upya sheria na nyaraka zinazokwenda kinyume na ulinzi usawa, na zisizosaidia maendeleo ya uchumi wa viwanda binafsi."

    Bw. Fu Zhenghua amesema hatua zitakazofuata ni kutekeleza utaratibu wa kutoa tangazo la utekelezaji wa sheria, kurekodi mchakato kamili wa utekelezaji wa sheria, upitishaji wa kisheria kwa maamuzi muhimu ya utekelezaji wa sheria, ili kutoa uhakikisho wa kisheria wenye haki, kwa ajili ya maendeleo ya viwanda binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako