• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwango cha matumizi cha China kimeongezeka

    (GMT+08:00) 2018-11-12 19:05:59

    Thamani ya makubaliano yanayotazamiwa kufikiwa katika maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uingizaji bidhaa kutoka njeya China CIIE imefikia dola bilioni 57.83 za kimarekani, huku mauzo ya punguzo kubwa la tarehe 11/11 ya T-mall ikiweka rekodi ya mauzo ya dola bilioni 30.7 za kimarekani. Uwezo mkubwa wa manunuzi umeonesha uwezo mkubwa wa soko la China, ambao pia umeonesha zama ya kuongezeka kwa kiwango cha matumizi imefika.

    Mauzo ya punguzo kubwa la tarehe 11/11 yalianza Novemba 11 mwaka 2009. Kufuatia maendeleo ya miaka 10, mauzo hayo yemekuwa tamasha kubwa zaidi ya manunuzi inayoshirikisha dunia nzima, ambayo pia yanachukuliwa kuwa alama ya soko la matumizi la China. Mauzo ya mwaka huu yameweza kuenea kote duniani, na wateja wa nchi mbalimbali duniani wamefanya manunuzi kupitia majukwaa matatu ya AliExpress, Lazada na Daraz pamoja na wateja wa China.

    Tofauti na mwaka jana ni kwamba, mauzo ya mwaka huu yalianza siku moja baada ya kufungwa kwa maonesho ya CIIE. Waagizaji zaidi ya laki 4 kutoka ndani na nje ya China waliendelea kuonesha uwezo mkubwa wa kununua kwenye mauzo ya punguzo kubwa la tarehe 11/11, na wameyafanya mauzo hayo yaliyoingia katika mwaka wa kumi kuwa ya kimataifa zaidi.

    Kwa mfano katika jukwaa la T-mall la kimataifa, chapa zaidi ya elfu 20 kutoka nchi na sehemu 75 duniani zimeshiriki kwenye mauzo ya mwaka huu. Mazao ya kilimo ikiwemo parachichi kutoka Mexico, uduvi mwekundu kutoka Argentina, salmon kutoka Denmark yalipendwa na wateja, pia roboti ya kufagia, mashine za kuongeza unyevu kwenye hewa zimenunuliwa kwa wingi na wateja. Mauzo ya huduma za upimaji wa afya, uchunguzi na tiba ya kinywa pia yamezidi ya mwaka jana.

    Mbali na hayo, mauzo ya mwaka huu yameunganisha maduka ya mtandao wa Internet na maduka halisi na kuleta fursa kubwa kwa maduka halisi. Mtindo huo wa muungano maduka ya mtandao wa Internet na maduka halisi umekuwa njia muhimu ya kukidhi soko la matumizi na mahitaji mablimbali ya wateja.

    Hayo yote yamezidi makadirio ya wazinduzi wa mauzo hayo. Tangu mwaka 2009 hadi 2018, thamani ya mauzo ya bidhaa kwenye Mauzo ya punguzo kubwa ya tarehe 11/11 imeongezeka kutoka dola milioni 7.18 za kimarekani hadi dola bilioni 30.6 za kimarekani, huku chapa zinazoshiriki zikiongezeka kutoka 27 hadi laki 1.8. Mabadiliko ya mauzo hayo yameonesha mabaliko ya miundo ya matumizi ya wachina, na mchakato wa uchumi wa China kubadilika kuwa kiwango cha juu zaidi, pia yameonesha imani ya wachina kuhusu mustakabali wa uchumi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako