Hayo yalibainishwa na katibu wa kikundi cha ujasiriamali cha Amaanan kutoka wilaya ya Newala,Sharafa Mtutuma wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Mtutuma alisema kuwa kuna changamoto hiyo kwa wajasiriamali wanaozalisha korosho na kwamba wamejikuta wakikwama,hali ambayo inaweza kukwamisha malengo ya serikali ya kufikia uchumi wa viwanda.
Katibu huyo alisema kuwa,mbali na changamoto hizo,pia bidhaa mbazo wajasiriamli hao wanazalisha zinaweza zikakosa masoko ya uhakika.
Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Kilimo,Omary Mgumba,aliwataka wajasiriamali wadogo wadogo kuzalisha kwa wingi na kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa ili waweze kujiongezea kipato na kuondokana na umaskini.
Mgumba alisema kuwa serikali inatambua mchango unaotokana na vikundi vya wajasiriamali wadogo wadogo katika mapambano dhidi ya umaskini,hivyo upo umuhimu wa kuongeza mshikamano katika kuhakikisha kuwa vikundi vinapata mafunzo bora ili kuongeza ufanisi zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |