• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa uchukuzi atoa agizo shirika la reli liongeze safari wakati wa mgomo wa matatu

    (GMT+08:00) 2018-11-12 19:45:18
    Waziri wa uchukuzi nchini Kenya ameiliagiza shirika la reli nchini kuongeza idadi ya treni za kusafirisha abiria katika maeneo yote inakohudumu ili kukidhi mahitaji ya abiria wengi wanaotaabika kutokana na uhaba wa magari ya uchukuzi bara barani.

    Katika taarifa waziri wa uchukuzi James Macharia amelitaka shirika hilo kupunguza nauli kwa asilimia 10. Waziri Macharia amesema kuwa hatua hiyo pia itasaidia kufanikisha utekelezaji wa sheria maarufu za Michuki.

    Hii leo wananchi wengi wamelazimika kutembea kutokana na mgomo wa magai ya uchukuzi wa umma almaarufu matatu huku wenye magari hayo wakipinga utekelezwaji wa baadhi ya sheria za barabarani maarufu sheria za Michuki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako