• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Singida yazalisha asilimia 90 ya pamba yote inayolimwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-11-12 19:52:39

    Mikoa ya Simiyu,Shinyanga,Mwanza,na Singida imetajwa kuwa ndiyo nguzo ya uzalishaji wa pamba Tanzania.

    Akitoa taarifa katika mkutano wa wadau wa pamba ambao ulifanyika hivi karibuni,alisema mikoa hiyo pamoja na Mara,Tabora,na Kigoma,kwa pamoja inazalisha asilimia 90 ya pamba yote inayolimwa Tanzania.

    Hata hivyo alisema asilimia 80 ya pamba ya Tanzania inalimwa katika mikoa ya Simiyu,Shinyanga,Mwanza,na Singida.

    Mtunga ameeleza kuwa pamba nchini Tanzania,hulimwa hasa na wakulima wadogo kati ya 350,000 na 500,000 katika wilaya 49 za mikoa 17 ya bara.

    Mtunga liimwagia sifa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kutoa mkopo wa viuadudu msimu uliopita na kusema mkopo huo uliwanufaisha zaidi wakulima 600,000 wa pamba na kwamba umechangia vikubwa katika kuongeza mavuno kufikia tani 221,600.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako