• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Samatta aweka rekodi kali katika mechi 100

    (GMT+08:00) 2018-11-13 09:16:34
    Mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta jumapili amecheza mchezo wake wa 100 katika ligi kuu nchini Ubelgiji, huku timu hiyo ikiendeleza rekodi ya kutopoteza mechi msimu huu baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Royal Excel Mouscron.

    Kwa matokeo hayo, Genk inaendelea kuongoza ligi hiyo ikifikisha pointi 35 baada ya kutoka sare mechi 5 kati ya mechi 15 ilizocheza, nyingine zote 10 ikishinda.

    Kwa ujumla Samatta amefikisha mechi 129 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 51.

    Katika Ligi ya Ubelgiji pekee amefikisha mechi 100 na kufunga mabao 36, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 21 mabao 14.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako