• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA YAGAWA MAHINDI YA TSH65 MILIONI

    (GMT+08:00) 2018-11-13 19:25:39

    MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imegawa tani 145 za mahindi yenye thamani ya zaidi ya TSh65 milioni yaliyoingizwa nchini yakisafirishwa kuelekea nchini Rwanda kisha kutelekezwa.

    Meneja wa forodha mikoa ya Mbeya na Songwe, Jonamatha Nsindo alisema Jumapili kwamba mahindi hayo yaliingizwa nchini Novemba 2017, yalipofika mpakani Tunduma yalizuiliwa na mamlaka hiyo.

    Nsindo alisema baada ya kufikishwa mpakani hapo, msafirishaji wa mzigo huo, Salsbary Investment alitofautiana na mwenye mali na kusababisha mzigo kukaa mpakani kwa zaidi ya miezi mitatu yakiwa kwenye malori matano, hivyo aliyakabidhi kwa TRA.

    Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Nikodemas Mwangela alikabidhiwa mahindi hayo kisha kuyagawa kwa shule 18 za mkoa huo. Mkuu wa Sekondari ya Ileje, Julitha Mwaulambo alisema mahindi hayo yatasaidia kuokoa fedha za chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako