• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China umeendelezwa katika kiwango kichachofaa

    (GMT+08:00) 2018-11-14 17:14:43

    Msemaji wa idara ya takwimu ya China Bibi Liu Aihua leo hapa Beijing amesema kwa mujibu wa takwimu za uchumi kwa mwezi Oktoba, vigezo vikuu vya uchumi wa viko katika kiwango sahihi, hali ya kimsingi ya uendeshaji wa uchumi kwa utulivu haijabadilika, na mazingira ya kujiendeleza kwa utulivu ni ya kutosha.

    Takwimu zilizotolewa na idara ya takwimu ya China zimeonyesha kuwa, hivi sasa vigezo vikuu vya uchumi wa China vinadumu katika kiwango sahihi. Kwa mfano mwezi Oktoba, thamani ya ongezeko la viwanda imeongezeka kwa asilimia 5.9 kuliko mwaka jana wakati kama huo, kiwango cha uzalishaji wa sekta ya huduma kote nchini kimeongezeka kwa asilimia 7.2, na thamani ya jumla ya biashara ya rejareja ya bidhaa za matumizi imeongezeka kwa asilimia 8.6. na takwimu kutoka wizara ya raslimali watu na huduma za jamii ya China zinaonyesha kuwa, kati ya mwezi Januari hadi mwezi Oktoba mwaka huu, nafasi za ajira zinazoongezeka zimefikia watu milioni 12. Msemaji wa idara ya takwimu ya China Bibi Liu Aihua amesema, kwa sasa uendeshaji wa uchumi wa China unaonyesha mambo matatu.

    "Kwanza, uzalishaji na mahitaji ni tulivu kwa ujumla. Pili, hali ya ajira na bei ya bidhaa ni tulivu. Tatu, marekebisho ya miundo ya uchumi yametekelezwa kwa hatua madhubuti. Kutokana na mambo hayo matatu, kwa ujumla uchumi wa China umeendelezwa kwa utulivu. "

    Mambo yanayofuatiliwa zaidi ni kwamba, uwekezaji katika miundo mbinu kati ya mwezi Januari hadi mwezi Oktoba umeongezeka kwa kiasi kikubwa, na kufikia asilimia 3.7 kuliko mwaka jana wakati kama huo, likiwa ni ongezeko la asilimia 0.4 zaidi kuliko miezi tisa iliyopita. Hii ni mara ya kwanza kwa ongezeko la uwekezaji kwenye miundo mbinu kuongezeka ndani ya mwaka huu.

    Alipozungumzia mustakabali wa uchumi wa China, Bibi Liu Aihua amesema, China ina soko kubwa na raslimali watu nyingi ya watu zaidi bilioni 1.3, watu zaidi milioni 170 wamepata elimu ya juu na elimu ya ufundi, pia ina mfumo kamili wa viwanda na miundo mbinu inayoboreshwa siku hadi siku. Amesema,

    "kiwango cha mfumuko wa bei kiko chini, kiasi cha upungufu wa fedha pia kiko katika kiwango cha chini, kiasi cha deni la serikali kiko katika eneo la kufaa, akiba ya fedha za kigeni ni ya kutosha, hayo yote yanaonesha kuwa sera ya uchumi inaweza kutekelezwa kwa ufanisi, na inasaidia kuonesha uwezo wetu wa muda mrefu, na kuunga mkono uchumi wa China kuendelea kujiendeleza vizuri."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako