• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa maadhimisho ya miaka 10 ya APSCO

    (GMT+08:00) 2018-11-14 18:22:38

    Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa maadhimisho ya miaka 10 ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Anga za Juu wa Asia na Pasific (APSCO).

    Katika barua yake, rais Xi amesema anga za juu ni utajiri wa pamoja wa binadamu na ni jukumu la binadamu kutafiti, kuendeleza na kutumia anga hiyo kwa amani. Amesema China inapenda kuongeza juhudi kwa pamoja na nchi nyingine duniani kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kuboresha mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa katika anga za juu kwenye msingi wa usawa, kunufaishana, matumizi ya amani, na maendeleo jumuishi.

    Rais Xi amesema, APSCO na nchi wanachama wake wanachukua nafasi muhimu katika kuboresha ushirikiano wa karibu katika nyanja mbalimbali ikiwemo utafiti wa anga za juu, pamoja na maendeleo na matumizi ya teknolojia ya anga za juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako