• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Mkataba wa biashara wa TMEA kuendeleza mauzo ya nje

    (GMT+08:00) 2018-11-14 18:44:02
    Shirika la TradeMark East Africa (TMEA) limetangaza kuwa litawekeza $2.4 milioni nchini Rwanda (Rwf2.1 billion) ili kuwezesha biashara za ndani kuongeza uelewa wa kufikia masoko ya kimataifa.

    Mkataba huo ni sehemu ya $50 milioni (Rwf44.3 bilioni) ya mkataba wa maelewano kati ya serikali ya Rwanda na TMEA uliotiwa saini mwaka jana kuboresha uwezo wa biashara za ndani kuuza nje.

    Mkurugenzi wa TMEA nchini Rwanda,Patience Mutesi,alisema msaada huo utawezesha viwanda vya ndani kuzalisha bidhaa ambazo zinakidhi viwango vya kimataifa.

    Bi. Mutesi alisema sehemu kubwa ya ufadhili huo itatumika kutoa msaada kwa makampuni yanayouza bidhaa nje kuongeza uwezo wao wa mauzo.

    Alisema hiyo inaweza kuwa katika mfumo wa kuweka pamoja mikakati ya uuzaji nje,kuwapatia mafunzo kuhusu ubora wa masoko ambako wanauza bidhaa zao,na majukwaa ya masoko ambapo wanaweza kushiriki katika mauzo na ujumbe wa biashara kwa masoko muhimu.

    Rwanda imefanya mageuzi mbalimbali yanayolenga kujenga mazingira mazingira mazuri ya biashara,lakini uchumi unakabiliwa na upungufu wa biashara kutokana na sekta dhaifu ya uuzaji nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako